REAL MADRID 1-1 ATLETICO MADRID  (Real Madrid yashinda taji la 11 kwa mikwaju ya penati (5-3).
    Cristiano Ronaldo akinyanyua kombe la ubingwa ulaya kwa mara ya 3

             Mshambuliaji wa kimataifa Cristiano Ronaldo afunga penati ya mwisho ya ushindi na real madrid kutwaa kombe la ubingwa wa ulaya kwa mara ya 11

             Ilikua ni fainali ya kipekee katika uwanja wa SAN SIRO ambapo kipindi cha kwanza kilikuwa ni msiba kwa Atletico baada ya kufungwa goli na Sergo Ramos dakika ya 15,
mpira wa adhabu uliopigwa na Tony kroose,Bale kuongezea kasi kwa kichwa na kutua miguuni kwa Ramos na nyavu kitingishika .
                
 hadi kuelekea mapumziko real walikua  kifua mbele kwa bao 1-0.
        
           Kipindi cha pili  Pepe alimchezea faulo Torres na kusababisha penati ,lakini haikuwa bahati kwa Atletico madrid Antonio Griezman aligongesha besela na kukosa penati hiyo.

      Mabadiliko ya Diego Simeone yalizaa matunda baada ya kuingia  Carrasco mwenye umri wa miaka 22 raia wa kibelgiji na kufunga goli la kusawazisha 1-1 na kumfanya mwamuzi kuongeza dakika 20,na mpira huo kuisha bia kufungana kuelekea hatua ya matuta(penati).

        Mlinzi wa Atetico madrid Juan Fran alikosa penati kwa kugongesha mwamba upande wake wakushoto.

         Cristiano Ronaldo hakufanya makosa alipiga penati ya ufundi na kuipa ubingwa klabu ya Real Madrid 2016/20017
           
   



https://www.youtube.com/watch?v=0I7r90_hVug
Axact

MASHA GMG

Asante kwa kutembelea www.mashagmg.blogspot.com, endelea kuhabarika zaidi kila siku kwa kupata habari,Michezo,Burudani, Music na Video mbalimbali.

Post A Comment: