Baada ya Bunge la Tanzania kupitisha bajeti iliyoweka kodi ya ongezeko la thamani katika sekta ya utalii, maelfu ya watalii waliokuwa watembelee Tanzania kuanzia Julai mosi mwaka huu wamefuta safari zao na kuzua hofu ya utalii katika Tanzania kuporomoka.
Kufikia leo asubuhi kampuni kubwa za mawakala wa utalii jijini Arusha zimeripoti katika chama chao kuwa wageni zaidi ya 8000 wamekatiza safari na kupoteza kiasi dola milioni sita.
pia kumekuwa na hofu kubwa kwa wafanya kazi wa utalii kuwa wapoteza ajira zao kwa kipindi hichi endapo serikali itaendelea kutilia mkazo suala hili.
kwa asilimia kubwa mikoa ya Kaskazini inategemea haswa biashara ya utalii.
Baadhi za ofisi za utalii zafungwa hususa zile zilizokuwa zikitegemea watalii wanaofika nchini na kuanza kupatana nao bei..vile vile baadhi ya wafanya kazi wa hoteli waanza kupewa likizo za lazima huku madereva wa utalii kupunguzwa mpaka hali itakapokuwa shwari.
Post A Comment: