TRENDING NOW

NEWS

SPORTS

VIDEO

Vyuo kurudisha fedha za wanafunzi hewa.
Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako amesema wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu wasio na sifa wataondolewa bila kujali wapo mwaka wa ngapi na hata waliopo kazini wataondolewa kwa kuwa hao ndio wanatumia njia za mkato kwenda kupata kazi japokuwa hawana sifa. Waziri amevitaka vyuo vikuu kuchukua wanafunzi walio bora ili kuweka sifa ya ubora wa vyuo vyao Na kuhusu vyuo vilivyochukua fedha ambazo hazikustahili vitalazimika kurudisha fedha hizo na kisha kuchukuliwa sheria kwa waliohusika, amesema bado wanaendelea kugundua idadi kubwa ya wanafunzi mfu walioombewa fedha tangia waanze zoezi hilo na sasa wamefikia vyuo vitatu tu.
Baada ya Bunge la Tanzania kupitisha bajeti iliyoweka kodi ya ongezeko la thamani katika sekta ya utalii, maelfu ya watalii waliokuwa watembelee Tanzania kuanzia Julai mosi mwaka huu wamefuta safari zao na kuzua hofu ya utalii katika Tanzania kuporomoka. Kufikia leo asubuhi kampuni kubwa za mawakala wa utalii jijini Arusha zimeripoti katika chama chao kuwa wageni zaidi ya 8000 wamekatiza safari na kupoteza kiasi dola milioni sita.
pia kumekuwa na hofu kubwa kwa wafanya kazi wa utalii kuwa wapoteza ajira zao kwa kipindi hichi endapo serikali itaendelea kutilia mkazo suala hili.
kwa asilimia kubwa mikoa ya Kaskazini inategemea haswa biashara ya utalii. Baadhi za ofisi za utalii zafungwa hususa zile zilizokuwa zikitegemea watalii wanaofika nchini na kuanza kupatana nao bei..vile vile baadhi ya wafanya kazi wa hoteli waanza kupewa likizo za lazima huku madereva wa utalii kupunguzwa mpaka hali itakapokuwa shwari.
Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.
Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya penalti.
''Amemwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu'' alisema msemaji wa rais Macri. Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi. Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika. Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania. Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia. Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo. Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen. ''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
SERIKALI YA RUHUSU BUNGE KUANZA KURUSHWA LIVE REDIONI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye amesema serikali imekubali kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja kupitia redio nchini. Hapo Mwanzo, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye, alisema Televisheni ya Taifa imeacha kurusha LIVE kipindi cha Bunge kuanzia jana ili kubana matumizi. Na itakuwa ikirekodi baadhi ya matukio na kuonyesha usiku. Swala la kusitisha Matangazo ya live yalilalamikiwa sana na wabunge hasa wa akambi ya Upinzani.
JENGA HESHIMA YA NDOA YAKO KWA KUTUMIA NYANYA CHUNGU
Ngogwe au nyanya chungu ni mboga abayo inafahamika sana miongoni mwetu na baadhi yetu tumekuwa tukiitumia katika mlo. Leo nimeona nikuletee hizi faida mbili za matumizi ya nyanya chungu. Ngogwe au nyanya chungu husaidia sana katika kuongeza nguvu za uzazi kwa wanaume na inatibu pia wale wenye ugonjwa wa ngiri. Mbali na sifa hiyo ya ngogwe / nyanya chungu pia husaidia kuongeza stamina na uwezo wa kuvumilia na kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu kati ya mume na mke wote endapo watakuwa wanatumia nyanya chungu katika utaratibu unaotakiwa kitaalam (mchemsho) . Mbali na hayo, ngogwe ni dawa inayofanana na antibiotic, hivyo ni tunda zuri endapo likitumiwa mara kwa mara husaidia kuua vijidudu vya aina mbalimbali mwilini.
Faida ya nyanya chungu mwilini ni hizi Nyanya chungu au ngogwe ni tunda ambalo wengi tumekuwa tukilitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida zake kiafya. Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha afya ya mlaji. Nyanya chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi vikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuboresha afya ya mwili kwa ujumla. Ndani ya nyanya chungu pia kuna Vitamin K inayosaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu. Licha ya kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji, mboga hii ina madini ya chuma na potassium hivyo kusaidia uimara wa mifupa. Nyanya chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na magonjwa ya mara kwa mara. Mboga hii pia ni kinga inayoweza kumuepusha mlaji kupata maradhi ya moyo au tumbo kujaa gesi au hutoa kinga kwa wanaume wasipate na ugonjwa wa ngiri. Kwa wagonjwa wa kisukari, nyanya chungu ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha sukari mwilini, hivyo basi katika chakula chako ni muhimu sana kula nyanya chungu japo kwa wiki mara mbili au tatu kutokana na faida zake kama tulivyoainisha hapa.
UJUE MCHAICHAI Ni wengi wanaoutumia nakuufahamu mchaichai kamakiungo cha chakula jikoni nawengine hutumia kama dawa ya mbu.Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya. .
Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni. Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda.
Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli. Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na: KINGA DHIDI YA SARATANI Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.
MMENG'ENYO WA CHAKULA -Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi. Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali. KUSAFISHA FIGO NA MKOJO Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani. Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha. MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango. “Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,” MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU vilevile mchaichai una kazi ya kusafisha damu, hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu
KUZUIA KUHARISHA Mchaichai pia unaelezwa kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha ambapo una uwezo wa kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huo.
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia majani ya mmea huu kwa muda mrefu, ataweza kujiepusha kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani husaidia katika kulegeza nyonga ambazo hubana katika kipindi cha ujauzito na kufanya njia kuwa ndogo kuwezesha mtoto kupita, WENYE VIDONDA VYA TUMBO Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.
HUONGEZA CD4 Kwa wagonjwa wa ukimwi, mchaichai unaelezwa kuwa huongeza CD4 na inashauriwa kuwa ni vyema mgonjwa wa aina hiyo akapendelea kutumia zaidi mchaichai kuliko majani ya chai.
Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya siri za afya bora na kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na kiafya.. JINSI YA KUACHA PUNYETO…..{ MASTURBATION }
Punyeto ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote. FANYA YAFUATAYO.... 1. Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako..
2.Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
3. Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
4.Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
5. Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.
6. Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
7.Anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine: hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko, pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.