UJUE MCHAICHAI
Ni wengi wanaoutumia nakuufahamu mchaichai kamakiungo cha chakula jikoni nawengine hutumia kama dawa ya mbu.Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya. .
Mafuta ya mchachai
hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda.
Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli. Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza
kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:
KINGA DHIDI YA SARATANI
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai,
kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani.
Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion,
Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.
MMENG'ENYO WA CHAKULA
-Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha
utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu,
unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.
KUSAFISHA FIGO NA MKOJO
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.
MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao
wengi wao huchukulia kama chango. “Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya
uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”
MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU
vilevile mchaichai una kazi ya kusafisha damu, hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu
KUZUIA KUHARISHA
Mchaichai pia unaelezwa kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huo.
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia majani ya mmea huu kwa muda mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani husaidia katika kulegeza nyonga ambazo hubana katika
kipindi cha ujauzito na kufanya njia kuwa ndogo kuwezesha mtoto kupita,
WENYE VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo,
mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.
HUONGEZA CD4
Kwa wagonjwa wa ukimwi, mchaichai unaelezwa kuwa huongeza CD4 na inashauriwa
kuwa ni vyema mgonjwa wa aina hiyo akapendelea kutumia zaidi mchaichai kuliko majani ya chai.
Post A Comment: