Skeikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Mussa Salum amesema kuna mambo makubwa manne ya kuzingatia wakati wa kuoa mujibu wa sheria ya dini, mwanaume hapaswi kuoa kwa sababu ya uzuri,wa mwanamke, (nasibu) umaarufu wa ukoo wake, au uwezo wa mali.

Sheikh amebainisha kwamba mwanamume akioa kwa sababu tuu ya uzuri wa mwanamke uzuri unaweza ukapotea muda wowote, mtu akioa kwa sababu ya mali au umaarufu nao unaweza kuisha wakati wowote na mtu hawezi kuwa mwema kutokana na vitu hivyo.

Sheikh ameyabainisha hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na kituo cha redio cha East Afrika Radio jijini Dar es salaam leo.

Ameweka wazi kwamba kinachotakiwa kwa mwanamume kuangalia kabla ya kuoa ni jambo kubwa moja 'Dini' ambapo hii ndiyo huonyesha kama mtu anafuata sheria na kuwa na hofu ya Mungu.
Aidha amesisitiza kwamba na mwanamke anapaswa kuangalia aolewe na mtu ambaye ana maadili na Dini hapo ndipo ndoa inaweza kudumu.

Hata hivyo Sheikh ameweka bayana kwamba Mwenyezi Mungu hapendi mtu wa kuoa na kuacha kwa sababu ndoa imewekwa na mwenyezi Mungu na ndiyo maana mtu huwa na muda wa kutulia kwanza kabla ya kufanya maamuzi.

- EATV
Axact

MASHA GMG

Asante kwa kutembelea www.mashagmg.blogspot.com, endelea kuhabarika zaidi kila siku kwa kupata habari,Michezo,Burudani, Music na Video mbalimbali.

Post A Comment: